Mpasuko wa kisiasa kisiwani Zanzibar
14 Agosti 2007Matangazo
Kulingana na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, mazungumzo hayo ni danadana ndipo wakaamua kutangaza kuwa yamekwama. Viongozi wa vyama vya CUF na CCM walitia saini makubaliano ya kukamilisha mazungumzo hayo ifikapo Agosti 16. CCM kwa upande wake inasisitiza kuwa ndiyo iliyoanzisha mazungumzo hayo na haiwezi kupangwa ratiba. Wakaazi wa Visiwani Zanzibar na Bara wana hisia gani? Thelma Mwadzaya alizungumza na baadhi yao akianza na Zakia Omar.