1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mostovoy wa Urusi nje ya kikosi baada ya kuambukizwa Corona

11 Juni 2021

Mchezaji wa timu ya taifa ya Urusi Mostovoy atakuwa nje ya kikosi baada ya kuambukizwa Corona

https://p.dw.com/p/3ul6N
Euro 2020 Russland
Picha: Alexander Demianchuk/TASS/dpa/picture alliance

Winga wa timu ya taifa ya Urusi Andrei Mostovoy ameondolewa katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya mataifa ya Ulaya Euro 2020 baada ya kuambukizwa Covid-19. Soma zaidi  Michuano ya mataifa ya Ulaya Euro 2020 kung'oa nanga Juni 11 hadi Julai 11

Mostovoy ni mchezaji wa kwanza kuondolewa katika kikosi cha timu zitakazoshiriki mashindano hayo baada ya kupatikana na Corona.

Kupitia ukurasa wa twitter timu hiyo imeandika kuwa nafasi ya Mostovoy itachukuliwa na beki Roman Evgeniev kutokana na hali isiyoridhisha ya majibu ya kipimo cha corona cha PCR.

Frankreich empfängt seine Weltmeister
Mashabiki wa timu ya UrusiPicha: Getty Images/AFP/T. Samson

Siku ya Jumamosi Urusi ina miadi na Ubelgiji katika mechi yake ya kwanza ya michuano ya Euro 2020 huko St. Petersburg.

Mostovoy alijumuishwa katika kikosi cha Urusi mwaka jana. Alicheza mechi nane kati ya 11 za mwisho za timu hiyo kama mchezaji wa akiba.  Ujerumani, Ufaransa na Ureno Kundi moja Euro 2020     

Mechi pekee aliyocheza Evgeniev katika timu ya taifa ilikuwa ni dhidi ya Serbia ambapo Urusi ilipoteza kwa kufungwa mabao 5-0 mwaka jana.

Sweden na Uhispania pia zimeripoti visa vya wachezaji kupata maambukizi ya corona lakini bado hazijachukua uamuzi wa kuwabadilisha wachezaji walioathirika.

 

AP