MOSCOW: Wanamgambo wauawa nchini Russia.
4 Februari 2007Matangazo
MOSCOW
Wizara ya mambo ya ndani ya Russia imearifu kwamba maafisa wa usalama wamewaua wanamgambo wanne kwenye mji mmoja wa eneo la Ingushetia linalopakana na Chechnya.
Wakazi wengi wa eneo hilo ni wa kabila linalokaribiana na Wachechnya.
Msemaji wa wizara hiyo amesema watu hao waliuawa wakati wa mapigano ya risasi kwenye sehemu ya makazi.
Russia inaamini wanamgambo wanaounga mkono Chechnya kujitenga, wamejificha katika eneo hilo.