Moscow na Kyiv zalaumiana kila upande kufanya hujuma
12 Aprili 2024Taarifa ya wizara hiyo imedai droni zisizopungua nne za Ukraine zimeharibiwa kwenye mkoa wa Rostov na nyingine moja imedunguliwa ikijaribu kufanya hujuma katika mkoa wa mpakani wa Belgorod.
Madai hayo ya Urusi yametolewa wakati Ukraine nayo imesema mashambulizi ya droni za vikosi vya Moscow yamesababisha moto mkubwa kwenye kituo kimoja cha kufua umeme kusini mwa nchi hiyo na kuharibu miundombinu mingine.
Kyiv yaidhinisha mswada wa kuwaajiri watu jeshini wakati Moscow ikiishambulia miundo mbinu ya umeme
Katika ujumbe uliotumwa kupitia mtandao wa Telegram, jeshi la Ukraine limesema mashambulzii hayo yameyalenga majimbo ya Kherson na Dnipropetrovsk. Yameripotiwa katikati mwa miito inayotolewa na viongozi wakuu wa Ukraine wanaoyataka mataifa washirika kutuma silaha zaidi nchini humo kuvisadia vikosi vyake kujilinda mbele ya ubabe wa vikosi vya Urusi.