1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Jeshi la majini la Russia limeanza kazi ya kuiokoa nyambizi yake.

6 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEnQ

Jeshi la majini la Russia limeanza kushusha vifaa vya kuivuta nyambizi yake iliyonaswa chini ya bahari, mita 190 umbali kidogo kutoka pwani ya bahari ya Pacific nchini humo, kwa muda wa siku tatu zilizopita.

Wafanyakazi wa uokozi kutoka Marekani na Uingereza wakiwa na vifaa vya kutembea chini ya bahari pamoja na wataalamu wamekwenda katika eneo hilo katika juhudi za uokozi.

Watu saba ambao wamo katika nyambizi hiyo wameshusha nyuzi joto katika meli hiyo hadi nyuzi joto tano Celcius na wako katika giza katika juhudi za kupunguza matumizi ya hewa ya Oxygen ambayo binadamu anatumia ili kuweza kuishi. Maafisa wa jeshi la majini wanasema kuwa watu hao huenda wanayo hewa hiyo ya Oxygen inayotosha hadi kesho Jumapili.