1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MONTEREY: Amerika yahimizwa kuwa na biashara huru

13 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFjf
Viongozi wa Marekani,Canada na Mexico wamewataka viongozi wenzao wa nchi za Kusini na Amerika ya Kati kukaribisha biashara huru. Wito huo umetolewa katika Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Amerika ambao umeanza huko Monterey nchini Mexico hapo jana.Rais George W Bush wa Marekani amesema serikali yake imeajizatiti kuanzisha eneo huru la biashara la Amerika kwa kuwa ni njia nzuri ya kupambana na umaskini.Serikali ya Washington inataka kuwekwa kwa tarehe ya mwisho ya kuanzishwa kwa eneo hilo huru ifikapo Januari Mosi mwakani.Lakini Brazil na Venezuela zimesema mkutano huo wa Viongozi juu ya masuala ya fedha sio mahala pa kujadili masuala hayo. Serikali ya Marekani pia inataka kutojumuishwa kwa serikali ambazo zinatambulikana kuwa za rushwa katika Jumuiya ya Mataifa ya Amerika hatua ambayo imepingwa na mataifa kadhaa ya Amerika ya Kusini.