1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mo Ibrahim: Nchi tajiri ziache kujiwekea chanjo ya COVID-19

9 Juni 2021

Bilionea na mfadhili Mo Ibrahim amekosoa vikali hatua ya mataifa tajiri kujilimbikizia chanjo ya COVID-19 na kutoa mwito wa usawa katika mgawo wa chanjo hizo

https://p.dw.com/p/3uewQ
Mo Ibrahim | britisch-sudanesischer Mobilfunkunternehmer
Picha: Hollie Adams/AFP/Getty Images

Mo ametoa wito kwa jamuia ya kimataifa kutekeleza kwa vitendo matamko yao kuhusiana na usawa katika mgawo wa chanjo hizo wakati bara la Afrika likibaki nyuma.

Ibrahim anayetambulika kama kioo cha masuala ya utawala bora kote barani Afrika ameyaambia mataifa hayo tajiri kuacha ukasuku na kutekeleza kwa vitendo yale wanayoyasema na kuongeza kuyaambia angalau yatoe kiasi kidogo kwa ajili ya wafanyakazi walio mstari wa mbele katika afya barani humo.

soma zaidi: Bara la Afrika linahitaji haraka chanjo za COVID-19

Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO limesema wiki iliyopita kwamba upelekaji wa chanjo ya COVID-19 barani Afrika unakaribia kusimama kabisa katika wakati ambapo baadhi ya mataifa yanakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.  

Afrika imetoa dozi milioni 31 tu kati ya idadi jumla ya watu bilioni 1.3, ingawa ni watu milioni 7 waliopata dozi kamili ya chanjo.