1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa ujasusi Ethiopia ateuliwa naibu waziri mkuu

8 Februari 2024

Wabunge wa Ethiopia hii leo wameidhinisha uteuzi wa mkuu wa ujasusi, Temesgen Tiruneh, kuwa naibu waziri mkuu.

https://p.dw.com/p/4cAhH
Waziir Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.
Waziir Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.Picha: Fana Broadcasting Corporate S.C.

Wabunge pia wamemuidhinisha Atske Selassie, balozi wa zamani wa Ethiopia katika Umoja wa Mataifa na sasa mshauri wa kidiplomasia wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed, kuwa waziri wa mambo ya nje.

Nyadhifa hizo mbili awali zilishikiliwa na Demeke Mekonnen, ambaye aliachishwa kazi kama makamu wa rais wa chama tawala cha Abiy, cha Prosperity mwishoni mwa mwezi uliopita katika hatua ambayo iliashiria uteuzi uliodhinishwa leo.

Atakayechukua nafasi ya Temesgen kama mkuu wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi na Usalama bado hajatangazwa.