1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Mkuu wa shirikisho la soka Ufaransa achunguzwa

18 Januari 2023

Waendesha mashtaka nchini Ufaransa, wanamchunguza mkuu wa shirikisho la soka nchini humo Noel Le Great kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kingono.

https://p.dw.com/p/4MLo1
Fußball WM Katar | Präsident der FFF | Noel Le Graet
Picha: Christophe Ena/AP Photo/picture alliance

Waendesha mashtaka nchini Ufaransa, wanamchunguza mkuu wa shirikisho la soka nchini humo Noel Le Great kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kingono.

Tuhuma hizo zimetolewa na wakala wa soka la wanawake Sonia Souid, na wafanyakazi kadhaa wa shirikisho hilo. Inadaiwa manyanyaso hayo yalifanyika kati ya mwaka 2013 na 2017.

Waendesha mashtaka walianza uchunguzi wao dhidi yake jana. Lakini hiyo ni hatua ya kwanza kabla ya uwezekano wa mashtaka rasmi kufunguliwa dhidi yake.

Souid anamtuhumu mkuu huyo wa soka la Ufaransa kwa mienendo isiyofaa ya kingono kwa miaka mitano alipokuwa akijaribu kuanzisha uhusiano wa kikazi naye, ili kukuza soka la wanawake.

Amedai matendo yake yalimfanya afikirie kuacha kazi kama wakala wa mchezo wa soka.

Waziri wa michezo wa Ufaransa Amelie Oudea Castera, aliamuru uchunguzi kufanywa dhidi ya shirikisho hilo.