Mkuu wa NATO asema Ukraine bado haijachelewa kushinda vita
29 Aprili 2024Katika mkutano wa wanahabari nchini Ukraine Stoltenberg amesema Ukraine imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa silaha kwa miezi kadhaa, lakini hajachelewa kujiimarisha na kupata ushindi kwani msaada zaidi uko njiani.
"Kwa miezi kadhaa, Marekani haikuweza kukubaliana kuhusu kifurushi cha msaada kijeshi, na washirika wa Ulaya wameshindwa kutoa silaha kwa kiwango tulichoahidi. Ukraine imekuwa na uhaba wa silaha. Hii hiyo ina maana kwamba makombora machache na droni za Urusi zimedunguliwa na Urusi imepata mafanikio makubwa kwenye mstari wa mbele wa vita. Lakini bado Ukraine haijachelewa kushinda. Msaada zaidi uko njiani," amesema Stolteberg.
Akizungumzia msaada uliosubiriwa kwa muda mrefu, Zelensky alisema baadhi ya "vitu" vimeanza kuwasili lakini alikataa kutoa maelezo zaidi.