Mkuu wa IAEA akaribisha uamuzi wa Iran kuhusu mpango nyuklia
21 Novemba 2024Matamshi hayo aliyatoa katika mkutano wa IAEA mjini Vienna, Austria, huku mataifa yenye nguvu ya Ulaya na Marekani yakiwasilisha azimio la kuikemea Iran kwa ushirikiano wake mbaya na IAEA.
Soma pia:Iran yaonya azimio la nchi tatu za Ulaya ndani ya IAEA litavuruga mambo
Akizungumza na waandishi habari, Grossi alikaribisha kile alichokiita "hatua thabiti” ya Iran kukubali kuweka ukomo kwenye mpango wake wa urutubishaji madini ya urani.
Na kufuatia ripoti za uharibifu kwenye mpango wa nyuklia wa Iran uliosababishwa na shambulizi la Israel, Grossi ametoa wito wa sheria ya kimataifa kuheshimiwa. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliliambia bunge la Israel Jumatatu wiki hii kuwa sehemu ya mpango wa nyuklia wa Iran iliharibiwa katika shambulizi la kijeshi la Israel mwezi Oktoba.