UchumiUfaransa
Mkutano wa kilele wa Paris kujadili ufadhili wa kimataifa
19 Juni 2023Matangazo
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema mkutano huo wa Kilele wa Mkataba Mpya wa Kifedha wa Kimataifa utakaoanza siku ya Alhamisi, unalenga kujenga "makubaliano mapya" ili kufikia malengo jumla kukabiliana na umaskini, kuzuia ongezeko la joto duniani na kulinda bayoanuai.
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao kutoka mataifa zaidi ya 50 akiwemo Rais wa Kenya William Ruto na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, pamoja na Waziri Mkuu wa Barbados Mia Mottley, watajadili kuhusu mtazamo mpya wa kimuundo wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia.
AFP