1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa Asia bila ya muwafaka wa India na Pakistan:

3 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFmb

NEW DELHI: Waziri Mkuu wa India Atal Bihari Vajpayee amesema hakuna uwezekano wa kufikiwa muwafaka kati yake na Rais wa Pakistan Pervez Musharraf katika Mkutano ujao wa Kilele wa Nchi za Asia. Lazima utumie vilivyo wakati ili kuufanikisha Mkutano wa Kilele wa Kimkoa wa Jumuiya ya Nchi za Asia ya Kusini unaoanza hapo Jumapili ya kesho mjini Islamabad, Bwana Vajpayee alisema katika televisheni ya India. Viongozi hao wawili, Vajpayee na Musharraf walikutana mara ya mwisho mwaka 2001 nchini Nepal. Mpaka sasa madola hayo mawili ya kinyuklea hayana uhusiano mzuri. Ziara yake hiyo ya kwenda kuhudhuria mkutano wa Islamabad ni ziara ya kwanza ya Waziri Mkuu wa India Vajpayee nchini Pakistan tangu mwaka 1999. Mkutano huo wa siku tatu utahudhuriwa pia na viongozi wa Bangladesh, Sri Lanka, Nepal, Bhutan na Malediva.