1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa CDU wafunguliwa.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWJa

Hannover. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amefungua rasmi kikao cha siku mbili cha kila mwaka cha chama cha Christian Democratic Union mjini Hannover. Chama cha CDU kinapanga kuimarisha nafasi yake wakati wa mkutano huo na kujiweka katika nafasi ya kati katika siasa za Ujerumani wakati kikitaka kujiweka mbali na washirika wake katika serikali ya mseto chama cha Social Democratic, SPD. Chama cha SPD kimeelemea zaidi katika mrengo wa shoto katika mkutano wake mwezi wa Oktoba , wakirejesha nyuma mageuzi ya soko la kazi ambayo yameonekana kuuweka uchumi imara kabisa katika Ulaya katika njia sahihi. Chini ya uongozi wa Merkel , chama cha CDU kinaongoza katika maoni ya wapiga kura kwa asilimia 39 dhidi ya asilimia 26 za SPD. Kansela amekwisha tumikia nusu ya muda wake wa miaka minne katika utawala , na uchaguzi unatarajiwa kufanyika 2009.