1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mkutano muhimu wa chama tawala cha China waanza Beijing

15 Julai 2024

Chama tawala cha Kikomunisti nchini China, kimeanza mkutano wake mkuu muhimu unaoongozwa na rais Xi Jinping ukilenga kujadili hasa suala la uchumi wa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4iIXX
China I Xi Jinping - Mkutano wa chama tawala
Rais Xi Jinping wa China.Picha: Ng Han Guan/AP/picture alliance

Mkutano huo unafanyika mjini Beijing katika wakati ambapo China imeshuhudia ukuaji mdogo wa kiuchumi kuliko ilivyotarajiwa katika robo ya pili ya mwaka wa kiuchumi.

Mkutano huo unatarajiwa kujadili namna ya kukabiliana na kuporomoka kwa ukuaji wa uchumi, kutokana na kushuhudiwa mgogoro wa madeni katika sekta ya biashara ya ujenzi wa majumba, kupungua ununuaji wa mahitaji na kuongezeka kwa idadi ya wazee.

Mivutano ya kibiashara na Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya pia imechangia kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi wa China ambapo takwimu rasmi zinaonesha kwamba nchi hiyo ininayoshika nafasi ya pili kiuchumi duniani uchumi wake ulistawi kwa asilimia 4.7 pekee katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW