1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mke wa rais wa zamani wa Marekani Rosalynn Carter aaga dunia

20 Novemba 2023

Mke wa rais wa zamani wa Marekani Rosalynn Carter, ambaye Rais Jimmy Carter alimuita "sehemu ya mwili wangu" kutokana na mchango mkubwa aliokuwa nao katika utawala wake, ameaga dunia jana akiwa na umri wa miaka 96.

https://p.dw.com/p/4Z9lo
Rais wa Marekani l Mke wa Rais - Rosalynn Carter
Mke wa rais wa zamani wa Marekani Rosalynn CarterPicha: Ron Harris/AP/picture-alliance

Kulingana na kituo cha Carter, Rosalynn Carter ambaye katika siku za hivi karibuni alikuwa ameanza kupokea huduma za uangalizi maalum nyumbani kwake Georgia, alifariki kwa amani akiwa kando na familia yake.

Mnamo mwezi Mei, familia yake ilifichua kwamba bi Rosalynn Carter alikuwa na ugonjwa wa kupoteza fahamu.

Jimmy Carter mwenye umri wa miaka 99, pia anaendelea na matibabu ya nyumbani na kutunzwa na wahudumu wa afya baada ya kuamua mnamo mwezi Februari, kwamba hataki tena matibabu ya ziada ya hospitali.

Jimmy Carter, alihudumu kama rais wa Marekani kutoka mwaka 1977 hadi 1981. Carter na Rosalynn walifunga ndoa mnamo mwaka 1946 wakati huo Carter akiwa na umri wa miaka 21 wakati bi Rosalynn alikuwa na umri wa miaka 18.

Bi Rosalynn ameacha watoto wanne, wajukuu 11 na vitukuu 14.