1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGabon

Mke wa rais wa zamani wa Gabon afungwa jela

12 Oktoba 2023

Mke wa rais wa Gabon aliyeondolewa madarakani Ali Bongo Ondimba, amefungwa jela kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wakili wake.

https://p.dw.com/p/4XSz4
Sylvia Bongo Ondimba, amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu mapinduzi mwishoni mwa mwezi Agosti.
Sylvia Bongo Ondimba, amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu mapinduzi mwishoni mwa mwezi Agosti.Picha: Gabriel Bouys/AFP

Sylvia Bongo Ondimba Valentin amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu kulipotokea mapinduzi mwishoni mwa mwezi Agosti.

Sylvia anayetuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma, alifungwa jela Jumatano jioni.

Wakili wake Francois Zimeray amelaani hukumu hiyo aliyoitaja kuwa ni utaratibu wa kiholela na haramu.

Mke huyo wa rais Bongo alishitakiwa Septemba 28 kwa utakatishaji wa fedha na kughushi nyaraka. Viongozi wa mapinduzi wanamtuhumu rais wa zamani wa Gabon na wapambe wake kwa kughushi matokeo ya uchaguzi.

Pia wanamtuhumu Sylvia na mtoto wake wa kiume Nourredin Bongo Valentin kwa kumdanganya rais huyo wa zamani, ambaye hajapona kabisa ugonjwa wa kiharusi alioupata mwaka 2018.