1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili ya mahujaji 28 waliofariki kwa ajali yawasili Pakistan

24 Agosti 2024

Miili ya mahujaji 28 waliofariki dunia baada ya kupata ajali katikati mwa Iran imerejeshwa Pakistan. Mahujaji hao walikuwa safarini kwenda Iraq kuhiji katika ibada muhimu ya Waislamu wa dhehebu la Shia.

https://p.dw.com/p/4jsR8
Pakistan
Miili ya mahujaji 28 waliofariki kwa ajali yawasili PakistanPicha: Rizwan Tabassum/AFP/Getty Images

Kulingana na televisheni ya taifa ya Iran, Basi walilokuwa wakisafiria lililokuwa na jumla ya abiria 51lilipinduka na kuwaka moto Jumanne usiku katika kituo cha ukaguzi kwenye mkoa wa Yazd. 

Kulingana na mkuu wa idara ya kukabiliana na majanga wa mkoa wa Yazd, miongoni mwa waliokufa kwenye ajali hiyo ni wanawake 11 na wanaume 17.

Miili yao iliwasili Ijumaa usiku katika mji wa Jacobabad ambako wengi wao ndiko walikoanzia safari. Mkuu wa usalama barabarani wa Iran, alikitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni hitilafu katika breki za basi katika njia yenye mwinuko mkali.