1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo ya Olimpiki ya mjini Tokyo kufanyika mwakani

22 Julai 2020

Michezo ya Olimpiki ya mjini  okyo inaweza  kufanyika  tu mwaka  ujao iwapo hali ya virusi vya  corona  itakuwa  nzuri hadi  wakati  huo, kulingana na kamati ya matayarisho.

https://p.dw.com/p/3fhae
Japan Tokio Olympische Spiele verschoben
Picha: AFP/C. Triballeau

Michezo ya Olimpiki  ya mjini  Tokyo inaweza  kufanyika  tu mwaka  ujao iwapo hali ya virusi vya  corona  itakuwa  nzuri hadi  wakati  huo, mkuu  wa kamati ya matayarisho Yoshiro Mori  alikiambia  kituo cha  utangazaji  cha  NHK Jumatano.

Mori  amesema  haiwezekani  kuendesha  michezo  hiyo iwapo  hali itaendelea  kuwa  kama  ilivyo, na  kuongeza hafikiri  iwapo  hali  hii  itaendelea  kwa  mwaka  mwingine.

Michezo hiyo ambayo  ilikuwa  kimsingi  ifunguliwe siku  ya Ijumaa ,  iliahirishwa  mwezi Machi kwa miezi 12 kutokana na  janga  la  virusi  vya  corona.

Mji  wa  Tokyo  hivi  karibuni  umeshuhudia  idadi ya maambukizi ya  ugonjwa  wa  COVID-19 ikiongezeka tena. Mori amesema  kuwa  upatikanaji wa  chanjo ndio itakuwa ufunguo wa kufanyika  michezo  hiyo mwaka  2021, na iwapo  michezo  hiyo  itafanyika  ama la  itategemea  iwapo binadamu  wataweza kulishinda  janga  hilo.