1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michakato ya kuundwa miungano ya siasa Afrika Mashariki

Josephat Charo12 Juni 2020

https://p.dw.com/p/3dgz7

Huku Tanzania ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu wa 2020 chama cha upinzani cha ACT Wazalendo kimekiandikia chama kikuu cha upinzani CHADEMA kutaka ushirikiano kama ilivyokuwa wakati wa uchaguzi uliopita ambapo CHADEMA kilishirikiana na chama cha wananchi CUF na chama cha NCCR Mageuzi katika muungano wa UKAWA. Maoni mbele ya Meza ya duara leo yanaangalia michakato ya kuundwa miungano ya siasa barani Afrika hasa Afrika Mashariki, na kujikita pia katika yale yanayoendelea hivi sasa Tanzania kuelekea uchaguzi. Mwendesha kipindi ni Josephat Charo.