1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michael Jackson hana hatia

14 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3n

Mwanamuziki mashuhuri ulimwenguni Michael Jackson ametakaswa na mashtaka yote 10 dhidi yake..Michael Jackson alifunguliwa mashtaka tangu january iliyopita kwa madai ya kumnajisi mtoto,kumlevya ,na kumshikilia mamaake kwa nguvu katika kasri lake huko Neverland.Mamia ya mashabiki waliokua waakifuatilizia tangu mwanzo kesi hiyo,walihanikiza kwa vilio vya furaha hukmu ilipotolewa.Njiwa weupe walirushwa hewani kama ishara ya amani.Daima Michael Jackson alikua akisema hana hatia.