1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MIAMI: Raia wa Cuba washangilia

1 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDPu

Raia wa Cuba wanaoishi uhamishoni nchini Marekani, wamejitokeza kwa wingi katika barabara za Miami na Florida, wakicheza na kushanguilia waliposikia kwamba rais wao, Fidel Castro, amempa madara kakake, Raul Castro, kwa muda baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye utumbo.

Baadaye leo nderemo hizo ziliisha na watu wakaanza kusubiri kwa wasiwasi mkubwa kusikia habari juu ya hali ya afya ya rais Castro. Wahamiaji wengi wa Cuba nchini Marekani, wanamuona Castro kama dikteta katili ambaye kuondoka kwake kutaifungulia mlango enzi mpya ya demokrasia nchini Cuba.

Wakati huo huo, rais wa Venezuela, Hugo Chavez, akiwa ziarani nchini Vietnam, amemtakia afueni ya haraka rais Fidel Castro. Rais Chavez amesema ´Viva Fidel Castro´ na kumuombea apone na aishi milele.