1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfumo na kazi ya Bunge la Ujerumani, Bundestag

Schiffer, Hanno27 Septemba 2009

Kazi ya Bunge la Ujerumani, Bundestag

https://p.dw.com/p/Jpxy
Spika wa bunge la Ujerumani, Nobert lammert, akihutubia bungePicha: AP

Kazi ya bunge la Ujerumani ni sawa na mabunge mengine duniani ambayo ni kujadili, kutafakari na kupitisha sheria mpya.

Pamoja na kupitisha sheria bunge hilo linapitisha bajeti ya nchi kila mwaka.

Wabunge, yaani wawakilishi wa umma wanachaguliwa kila baada ya miaka minne. Idadi yao inafikia 600.

Kazi za bunge zinafanyika katika kamati kadhaa na kila chama kina wawakilishi wake bungeni. Uwakilishi wa wabunge hao kattika kamati mbalimbali unategemea na idadi ya kura ambazo kila chama kilifanikiwa kupata katika uchaguzi. Mijadala juu ya miswada ya sheria inafanyika kwenye kamati hizo.

SPIKA:

Shughuli za bunge zinaendeshwa na Spika .Baada ya rais wa jamhuri,Spika ndiye anayeshika nafasi ya pili ya juu katika dola,yeye pia ni kama mkuu wa serikali.

Spika anatoka kwenye chama chenye uwakilishi mkubwa zaidi bungeni.

Yeye ndiye anaeongoza vikao vya bunge na anahakikisha kwamba sheria za uwakilishi wa umma zinafuatwa.

SERIKALI ZA MAJIMBO,BUNGENI :

Serikali za majimbo pia zinawakilishwa bungeni.

Majimbo yote 16 ya Ujerumani yanashiriki katika kupitisha sheria kwenye Barazaa ,la wawakilishi.

Baraza hilo linatokana na mawaziri wakuu wa majimbo yote pamoja na mawaziri wa majimbo hayo.Uwakilishi wa jimbo katika baraza la wawakilishi unategemea na idadi ya watu wa jimbo husika.

Jimbo dogo kama la Bremen lililopo kaskazini mwa Ujerumani lina wawakilishi watatu kwenye baraza hilo. Jimbo kubwa la Bavaria lina wajumbe sita kwenye Baraza la wawakilishi.

Kabla ya kupitishwa na kuwa sheria, mswada unapitia hatua kadhaa. Jukumu la kupendekeza sheria ni la Bunge, Baraza la wawakilishi na serikali.

Kamati za bunge zinazingatia maudhui ya sheria.Wakati wa kupiga kura kila mbunge ana haki ya kushiriki kulingana na imani yake binafsi,lakini aghalabu wabunge hupiga kura kulingana na msimamo wa vyama vyao.

LENGO:Lengo ni kudhihirisha msimamo wa pamoja ya kila chama na kusisitiza maslahi ya kisiasa ya kila chama- mchakato unaoitwa nidhamu ya chama.Hata hivyo nidhamu hiyo haina maana ya kuwalazimisha wabunge kwenye kinyume na maadili ya uhuru-jambo hilo haliruhusiwi.

Baada ya sheria kupitishwa kwenye bunge,sheria zinawasilishwa kwenye Baraza la wawakilishi

Deutschland Bundestag Bonn 1949 Erster Bundestag
1.Dt.Bundestag am 7.9.1949 Gruendung der Bundesrepublik Deutschland: Konstituierende Sitzung des ersten Deutschen Bundestages am 7. September 1949 in der ehemaligen Paedagogischen Akademie in Bonn (nach Wahlen vom 14. Mai 1949). - Eroeffnung der Sitzung durch Alters- praesident Paul Loebe. - Foto.Picha: picture-alliance /akg

Ikiwa Baraza la wawakilishi linakataa kuidhinisha sheria fulani basi itapelekwa mbele ya kamati ya usuluhishi.Ikiwa mwafaka unafikiwa ,bunge litalazimika kuamua tena. Baada ya hapo Baraza la wawakilishi pia linaamua tena.

Katika mfumo wa bunge nchini Ujerumani, pana sheria za aina mbili-

zile zinazohitajika ridhaa ya Baraza la wawakilishi -kwa kiingereza approval laws na zile zinazoweza kupitishwa bila ya ridhaa ya baraza hilo appeal laws.

Mwandishi/Hanno Schiffer.

Mfasiri/Mtullya.

Mhariri:Aboubakary Liongo