Mfalme wa Uingereza Charles III ahudhuria ibada ya misa
11 Februari 2024Mfalme huyo mwenye umri wa miaka 75 alipigwa picha akiingia katika Kanisa la St Mary Magdalene kwenye makaazi ya kifalme ya Sandringham, Mashariki mwa Uingereza, ambako anaishi kwa sasa.
Soma pia: Mfalme Charles III wa Uingereza agunduliwa na saratani
Kuonekana kwa mfalme huyo kunakuja baada ya yeye kutoa ujumbe hapo jana Jumamosi jioni akielezea "shukrani zake za dhati kwa salamu nyingi za kheri njema'' ambazo amepokea tangu tangazo la ugonjwa wake kutolewa siku ya Jumatatu.
Mfalme Charles atoa kauli ya kwanza hadharani tangu kutangazwa kuugua saratani
Charles aliongeza kuwa mawazo mazuri kama hayo ndiyo faraja kuu. Hii ilikuwa kauli yake ya kwanza tangu Kasri la Buckingham kusema kuwa ameanza matibabu ya "aina ya saratani," bila kutaja ni aina gani.
Soma pia. Sunak amtakia afua Mfalme Charles III anayeugua saratani
Charles amechukua mapumziko kwa muda usiojulikana ya kutekeleza majukumu ya umma ya kifalme lakini anaendelea kufanya kazi za kiutawala faraghani.