1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Charles akutana na familia ya Dedan Kimathi

2 Novemba 2023

Mfalme Charles wa tatu wa Uingereza alifanya kikao cha faragha na familia ya mpiganiaji uhuru wa vita vya Mau Mau nchini Kenya aliyeuwawa Dedan Kimathi.

https://p.dw.com/p/4YJUR
Mfalme Charles wa tatu wa Uingereza
Mfalme Charles wa tatu wa Uingereza Picha: LUIS TATO/REUTERS

Alifanya ziara hiyo siku moja baada ya mfalme huyo kuelezea kile alichokiita "masikitiko na majuto makubwa" ya yaliyotokea enzi za ukoloni. 

Ubalozi wa Uingereza umesema mkutano huo ulikuwa fursa ya mfalme Charles kusikia moja kwa moja kuhusiana na madhila waliyofanyiwa Wakenya wakati walipokuwa wakipigania uhuru. Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni mwenyekiti wa Chama cha Wakongwe wa Mau Mau.

Mfalme Charles III ahuzunishwa na maovu ya ukoloni bila kuwaomba radhi Wakenya

Mfalme Charles na mkewe Carmilla ambao wako nchini Kenya kwa ziara ya siku nne, hajaomba radhi kuhusiana na yaliyotendwa na Uingereza katika kipindi cha ukoloni nchini humo, kama ilivyotarajiwa na Wakenya wengi.