1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfalme Abdullah akataa pendekezo la kuwahamisha Wapalaestina

12 Februari 2025

Mfalme wa Jordan Abdullah II kwa mara nyingine amekataa pendekezo la kuwahamisha maelfu ya Wapalestina.

https://p.dw.com/p/4qMSc
USA Washington, D.C. 2018 | Präsident Donald Trump und First Lady empfangen König Abdullah II und Königin Rania von Jordanien
Picha: Win McNamee/Getty Images

Hii ni baada ya mazungumzo na  Rais Donald Trump wa Marekani, aliyetoa wito wa wakazi hao karibu milioni 2 kuondolewa kwenye eneo hilo lililoharibiwa na vita.

Kwenye mkutano na Trump, Abdullah alijitolea kuwachukua hadi watoto 2,000 kutoka Gaza wenye maradhi ya saratani ama wanaohitaji huduma za dharura za matibabu.

Lakini baada ya mkutano huo, kupitia mtandao wa X aliandika ujumbe akisisitiza  msimamo mkali wa Jordan dhidi ya hatua ya kuwahamisha Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi. Akaongeza kuwa huo ni msimamo wa pamoja wa mataifa ya kiarabu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Ahmed Aboul Gheit pia amelipinga wazo hilo akiliita lisilokubalika kwenye ukanda huo, huku China ikisema Gaza ni ya Wapalestina.