1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Messi atabaki Barcelona; hali inayoleta utata mpya

Sekione Kitojo
5 Septemba 2020

Lionel Messi hakuonekana katika mazowezi  ya klabu yake ya Barcelona leo Jumamosi(05.09.2020)licha ya uamuzi wa kubakia katika  klabu hiyo kwa makubaliano maalum, wamesema waandishi wa AFP wakihudhuria mazowezi hayo.

https://p.dw.com/p/3i2fF
Fußballspieler Lionel Messi nach niederlage gegen Bayern München 2020
Picha: picture-alliance/AP Images/M. Fernandez

Jogoo  huyo  nyota wa  Argentina alitangaza  siku  ya Ijumaa  kuwa  amelazimika  kubakia Barcelona, akidai  ni  baada  ya  rais wa klabu  hiyo Josep Maria bartomeu  kukiuka  kauli yake  kumwachia  aondoke.

Imekuja  siku  10 baada  ya  hali  ya  wasi  wasi  na  mvutano  wa mtikisiko wa  taarifa  yake kwa  njia  ya  fax iliieleza  Barcelona  kwamba  anataka  kuondoka.

Champions League | FC Barcelona - FC Bayern München | Lionel Messi
Mchezaji nyota wa Barcelona Lionel MessiPicha: picture-alliance/Sven Simon/F. Hörmann

Lakini  wakati  wachezaji  wengine ikiwa  ni  pamoja  na  Jordi Alba  na  Philippe  Coutinho waliwasili kwa  ajili  ya  mazowezi  hayo, Messi  alishindwa  kujitokeza  katika  uwanja  wa mazowezi  wa  Joan Gamper kwa  ajili  ya  mazowezi  ambayo  yameanza  leo asubuhi.(05.09.2020)

Jumapili  iliyopita Messi  kwa  makusudi mazima  aliepa kufanyiwa  vipimo vya lazima vya virusi  vya  corona ambavyo  wachezaji  wote  wa  barcelona  wanalazimika  kufanyiwa. Kwa mujibu wa  vyombo  vya  habari nchini  humo, Messi ni  lazima  kwanza apate uthibitisho kuwa hana  maambukizi  ya  COVID-19 na anaweza  kurejea katika  kikosi  hicho huenda Jumatatu.

Anaweza  baada  ya  hapo kuingia  katika  mipango ya  mchezo  wa  kwanza  wa  kocha mpya Ronald Koeman, mchezo  wa  kirafiki dhidi  ya  timu  ya  daraja  la  tatu  Nastic hapo Septemba 12.

Spanien F.C. Barcelona | Protest gegen den Abschied von Leo Messi
Mashabiki wakionesha mshikamano na nyota wao hata kama ametangaza kuondoka katika klabu hiyoPicha: picture-alliance/NurPhoto/A. Llop

Mazungumzo na vilabu vingine

Lionel Messi  anabakia  Barcelona lakini kwa  muda  gani? Messi  anaweza  kufanya mazungumzo  na  timu  nyingine  kuanzia Januari mosi na  kuondoka  katika  klabu  hiyo majira  ya  joto mwakani, wakati  mkataba  wake utakapomalizika na mara hii ataondoka  bila kulipiwa fedha  za  uhamisho. Hadi wakati  huo , Barca  inabidi  kutafuta  njia  ya  kumrejesha kundini  mchezaji  wake  huyo nyota, ambaye  hataki  tena  kucheza  katika  timu  hiyo.

Tangazo lake ambalo lilikuwa  na  viashiria  vya  uchungu siku  ya  Ijumaa  halikupokelewa kwa  sherehe, hata miongoni mwa  mashabiki, wengi  wao  waliunga  mkono  uamuzi  wake wa  kuondoka, wakipata ahueni  kidogo katika  wazo lake  la  kutafuta  mafanikio  sehemu nyingine.

Kulikuwa  na  ukimya  pia kutoka kwa wachezaji  wenzake, hakuna aliyeonesha  kumpa uungwaji mkono hadharani  ambao Luis Suarez na  Carles Puyol walitoa  wakati Messi alipoiambia  Barca  anataka  kuondoka.

Spanien F.C. Barcelona | Neuer Coach Ronald Koeman
Kocha mpya wa Barcelona Roland KoemanPicha: picture-alliance/AA/A. Puig

Hata  klabu  hiyo  pia  ilionekana  haina  hakika juu  ya  vipi kuangalia  tamko la  Messi. Ilichukua  karibu  masaa  matatu  kabla ya  picha  ya  Messi  kuingia  katika  jukwaa  lake  la mitandao  ya  kijamii, kukiwa  na  maneno chanya tu  ambayo  alizungumza  wakati  wa mahojiano  yake hapo  mapema, sio  kupitia  vyombo  rasmi vya  klabu hiyo, lakini kwa njia ya  Goal.

Shingo upande

"Nitatoa uwezo wangu wote. Mapenzi yangu kwa Barca hayatabadilika", ilisomeka.

Lakini  hata iwapo nia ya Messi ni safi, vipi hataweza  kubadilika kutokana  na  hili ? Uchungu wake ulionekana  wazi na  hisia zake zilikuwa  wazi.

Kama  rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu hakusimama katika njia  ya  Messi, alikuwa ameondoka, huenda  kwa  hivi  sasa  angekuwa  ana  sare ya  Manchester City na kufanya mazowezi  katika  uwanja  wa  Etihad.

Spanien F.C. Barcelona | Protest gegen den Abschied von Leo Messi
Mashabiki wakivalia sare za Barcelona wakimuaga nyota wao Lionel MessiPicha: picture-alliance/NurPhoto/Urbanandsport/J. Valls

Badala  yake  amelazimishwa  kubaki kinyume  na  matakwa  yake  na  kubakia  kama sehemu  ya  mradi  ambao  hana imani  nao  tena.

Nabaki hapa  kwasababu  rais  amesema  njia  pekee  ya  mimi  kuondoka  ni  kulipwaeuro milioni 700 katika  kifungu cha  kuachana, ambazo ni  vigumu kulipwa, ama  njia  nyingine  ni kwenda  mahakamani," Messi  alisema.