1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Meli ya uokozi ya Ujerumani yaokoa wahamiaji 200 Mediterania

1 Julai 2023

Meli ya kiraia ya uokoaji ya Ujerumani iitwayo Humanity 1, imewaokoa wahamiaji 200 waliokuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania karibu na kisiwa cha Lampedusa.

https://p.dw.com/p/4TIxp
Seenotrettungsschiff Humanity 1
Picha: Camilla Kranzusch/ROPI/picture alliance

Meli ya kiraia ya uokoaji ya Ujerumani iitwayo Humanity 1, imewaokoa wahamiaji 200 waliokuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania karibu na kisiwa cha Lampedusa. Katika opersheni zake, Humanity 1 ilikutana na mashua za wahamiaji zilizokuwa zikikabiliwa na dhoruba.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na shirika la kiutu la SOS lenye makao yake makuu mjini Berlin na linalomiliki meli hiyo, imeeleza kuwa baadhi ya wahamiaji waliookolewa kutoka kwenye mashua, wakionekana kudhoofika kupita kiasi au wakiwa na majeraha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni ya kwanza ya kuwaokoa wahamiaji iliyofanywa na meli ya Humanity 1, ilifanyika Alhamisi ikiwa na wahamiaji 197, na kwenye bandari ya Ortona nchini Italia ambako hata hivyo haikuruhusiwa kuingia kwenye bandari hiyo.