1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaDenmark

Meli ya Denmark iliyotekwa na maharamia yagundulika

31 Machi 2023

Meli ya mafuta ya Denmark iliyokuwa imetekwa nyara na maharamia imepatikana katika Ghuba ya Guinea, ila baadhi ya wafanyakazi wake wametekwa nyara

https://p.dw.com/p/4PXQj
Öltanker Monjasa Reformer
Picha: MONJASA/AFP

Haya ni kwa mujibu wa mmilki wa meli hiyo ya Monjasa. Meli hiyo iitwayo Monjasa Reformer iliyokuwa na wafanyakazi 16 wakati ilipovamiwa na maharamia mnamo Machi 25, ilipatikana katika pwani ya visiwa vya Sao Tome na Principe hapo jana.

Na sasa katika taarifa Monjasa imesema, maharamia hao walikuwa wameondoka na baadhi ya wafanyakazi kutoka kwenye meli hiyo wakati ilipopatikana.

Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa wafanyakazi waliookolewa wote wako salama katika mazingira salama na wanahudumiwa vyema. Hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu idadi ya waliotekwa nyara au uraia wao.