1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchakato wa kumtafuta mtetezi wa Urais visiwani Zanzibar

5 Julai 2010

Mwishoni mwa wiki kamati maalum ya Chama tawala cha mapinduzi, CCM, huko Visiwani Zanzibar ilikutana kuyajadili majina ya wanachama wao 11 wanaotaka kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/OBCb

Kati ya majina hayo kuna waziri kiongozi wa zamani, Dr. Mohammed Gharib Bilal; waziri kiongozi wa sasa, Shamsi Nahodha; makamo wa waziri kiongozi wa sasa, Ali Juma Shamhuna, na pia balozi Ali Karume, ndugu wa rais wa sasa wa Visiwani zanzibar, Amani Karume.

Othman Miraji punde amezungumza na Saleh Ferouz, naibu katibu mkuu wa Chama cha CCM upande wa Zanzibar, na alimuuliza kuhusu mchakato huo wa kumtafuta mtetezi wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM...

Mhariri:Mwadzaya,Thelma