1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbio za ubingwa wa Ujerumani zashika kasi

17 Aprili 2023

Pointi mbili tu ndizo zinazowatenganisha Bayern Munich na Borussia Dortmund katika jedwali la Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga baada ya timu zote mbili kushindwa kupata ushindi katika mechi zao mwishoni mwa wiki.

https://p.dw.com/p/4QCco
Bundesliga - Stuttgart - Dormund 15.04.2023
Picha: picture alliance/dpa

Dortmund walitoka sare mabao 3 na VfB Stuttgart ugenini huku Bayern wakizuiliwa sare ya bao moja na TSG Hoffenheim nyumbani kwao Allianz Arena.

Bayern walionekana kutokuwa na makali bila kuwepo kikosini kwa mchezaji nyota Sadio Mane ambaye alipewa marufuku ya mechi moja na klabu yake kwa utovu wa nidhamu.

Kocha wa Dortmund Edin Terzic alighadhabishwa na jinsi wachezaji wake walivyoupoteza uongozi wa mechi katika dakika za mwisho za muda wa majeruhi kwani ushindi katika mechi hiyo ungeipelekea timu hiyo kuwa sawa kipointi na Bayern ambao kwa sasa wana pointi 59 Dortmund wakiwa pointi mbili tu nyuma yao.

Chanzo: Jacob Safari/Reuters/AP