1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa Nchi za Kiarabu walaani filamu

29 Septemba 2012

Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Mataifa ya Kiislamu wametoa wito wa kuwekwa sheria dhidi ya uchochezi wa chuki za kidini, huku wakilaani filamu iliyotengenezwa Marekani inayoidhihaki dini ya Kiislamu.

https://p.dw.com/p/16HMI
REFILE - UPDATING CAPTION WITH IDENTITY OF PERSON BEING ESCORTED Nakoula Basseley Nakoula (2nd R) is escorted out of his home by Los Angeles County Sheriff's officers in Cerritos, California September 15, 2012. Nakoula, a California man convicted of bank fraud has been escorted to an interview with federal officers probing possible probation violations stemming from the making of an anti-Islam video that has triggered violent protests in the Muslim world, police said on Saturday. A Los Angeles County Sheriff's spokesman said Nakoula voluntarily left his home, accompanied by sheriff's deputies, to meet with the officers in the Cerritos Sheriff's Station. The obscure 13-minute English-language video, which was filmed in California and circulated on the Internet under several titles including "Innocence of Muslims," portrays Prophet Mohammad engaged in crude and offensive behavior. REUTERS/Bret Hartman (UNITED STATES - Tags: RELIGION CRIME LAW POLITICS)
Produzent des islamfeindlichen Films Die Unschuld der Muslime ist festgenommen wordenPicha: Reuters

Mawaziri kutoka Kundi la Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu - OIC lenye nchi wanachama 57, walisema haki ya kujieleza inapaswa kutumiwa kwa uwajibikaji.

Walitoa mwito kwa serikali kote ulimwenguni kuchukua hatua zote muhimu, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria dhidi ya matendo kama hayo ambayo husababisha uchochezi wa chuki, ubaguzi na ghasia kwa misingi ya kidini.

Kundi la Ushirikiano wa Kiislamu - IOC linataka hatua ichukuliwe dhidi ya uhasama wa kidini ulimwenguni
Kundi la Ushirikiano wa Kiislamu - IOC linataka hatua ichukuliwe dhidi ya uhasama wa kidini ulimwenguniPicha: AP

Mawaziri hao wa kundi la IOC walikutana pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambako filamu hiyo iliyotengenezwa nchini Marekani ilishutumiwa vikali, pamoja na mauwaji ya wanadiploamasia wanne wa Marekani waliouawa katika maandamano ya kupinga filamu hiyo nchini Libya.

Katika taarifa, mawaziri hao walilaani kile walichokitaja kuwa i „kutovumiliana, ubaguzi, unyanyapaa, chuki ya kidini na ukatili dhidi ya Uislamu“, kufuatia kutolewa kwa filamu iliyotengenezwa Marekani na vikaragosi vinavyomwonyesha Mtume Mohammed.

Mawaziri hao walitoa wito wa kuwepo uhamasisho wa kimataifa kuhusu athari za uchochezi wa chuki za kidini, ubaguzi na ukatili. Mtu anayedaiwa kutengeneza filamu hiyo, Nakoula Basseley Nakoula alikamatwa na kuzuiwa bila kupewa dhamana, siku ya Alhamis, katika mji wa Los Angeles kwa kukiuka kanuni za adhabu aliyopewa kuhusiana na kesi ya sakata ya kughushi benki. Nakoula amejificha kutoka machoni mwa umma kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita, kuhusiana na kilio cha umma kupinga filamu hiyo yenye dakika 13.

Mtengenezaji wa filamu iliyoibua kilio kote ulimwenguni, Nakoula Basseley Nakoula, yuko kizuizini chini ya ulinzi mkali
Mtengenezaji wa filamu iliyoibua kilio kote ulimwenguni, Nakoula Basseley Nakoula, yuko kizuizini chini ya ulinzi mkaliPicha: Reuters

Rais wa Marekani Barrack Obama alilaani filamu hiyo lakini akatoa wito wa kuheshimiwa uhuru wa kujieleza katika mkutano huo wa kila mwaka wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Mawaziri kadhaa wa nchi za Kiislamu walitoa mwito wa kutungwa sheria ya kimataifa ili kuzuia mashambulizi dhidi ya dini.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wau Uturuki Ahmet Davotuglu alisema ongezeko la idadi ya visa ambavyo vinadhihaki dini na vile vile watu wanaofuata dini kama hizo, sasa limesababisha athari kubwa kwa amani ya kimataifa na usalama.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo