1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa EU wagawika kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati

Angela Mdungu
14 Oktoba 2024

Mawaziri wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya waliokutana Luxembourg, siku ya Jumatatu wameonesha mgawanyiko kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati unaoendelea kati ya Israel na makundi ya Hezbollah na Hamas.

https://p.dw.com/p/4lmkL
Mawaziri wa Mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya
Mawaziri wa Mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wakiwa katika kikao chao.Picha: Francois Lenoir/European Union

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wamekutana nchini Luxembourg na kushindwa kuficha tofauti zao kuhusu mzozo unaoendelea mashariki ya kati.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Luxembourg, Xavier Bettel, amesema wazi kwamba Umoja huo sasa unakosa ushawishi na kwamba kuna mgawanyiko mkubwa kati ya mawaziri hao.

Katika majadiliano, baadhi ya mawaziri walilaumu mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, ambapo wanapambana na wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran.

Uingereza, ikiwakilishwa na waziri wa mambo ya kigeni, David Lammy, ilishiriki katika mkutano huo kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili. 

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Lammy.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Lammy.Picha: Maja Smiejkowska/REUTERS

“Usalama wa Uingereza na Ulaya hauwezi kuwa na mgawanyiko, iwe ni kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine au masuala makubwa ya Mashariki ya Kati. Ni muhimu kwa Uingereza na Ulaya kuwa thabiti, Lammy alisisitiza.”

Vikwazo dhidi ya Iran na Moldova

Katika mkutano huo, mawaziri wa Umoja wa Ulaya pia walitangaza vikwazo dhidi ya watu watano na kampuni moja kwa tuhuma za kujaribu kuiyumbisha Moldavia.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Ulaya kupunguza ushawishi wa Urusi barani Ulaya.

Waliowekewa vikwazo ni pamoja na gavana wa mkoa wa Gaga nchini Moldavia, Eugenia Gutful, na maafisa wengine waliohusika na shughuli za watu wanaotaka kujitenga katika eneo hilo.

Fahamu kuhusu uchaguzi wa Bunge la Ulaya

Soma pia: Rais wa Moldova aishutumu Urusi kupanga njama ya kuuangusha uongozi wake

Aidha, mawaziri hao walitangaza vikwazo dhidi ya naibu waziri wa ulinzi wa Iran, Sayed Hamzeh Ghalandari, na maafisa wa bunge wa Iran.

Vikwazo hivi vinatokana na tuhuma za kushiriki katika kupeleka Urusi droni, makombora, na vifaa vingine vinavyotumika katika vita dhidi ya Ukraine.

Ghalandari na maafisa sita wa bunge wamepigwa marufuku kusafiri katika Umoja wa Ulaya, na mali zao zimeshikwa.

Umoja wa Ulaya pia umetangaza kuzishikilia mali za mashirika ya ndege ya Iran, Mahan na Saha, yaliyotumika kupeleka droni na makombora yaliyotengenezwa na Tehran.