1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri Blinken na Lammy waapa kuisaidia zaidi Ukraine

11 Septemba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Uingereza David Lammy wameahidi kuisadia Ukraine hadi itakapopata ushindi katika vita vyake na Urusi.

https://p.dw.com/p/4kWEE
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza na Marekani, Antony Blinken na David Lammy
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza na Marekani, Antony Blinken na David LammyPicha: Mark Schiefelbein via REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Uingereza David Lammy wameahidi kuisadia Ukraine hadi itakapopata ushindi katika vita vyake na Urusi. Wanadiplomasia hao wa ngazi za juuwamesema ziara yao ya pamoja mjini Kiev, inatuma ujumbe mzito, unaoonesha kwamba wanataka kuyaona mafanikio ya Ukraine na wako tayari kuisadia ili isimame yenyewe kijeshi, kiuchumi na kidiplomasia. Blinken, Lammy wamefanya mazungumzo na mwenzao wa Ukraine mjini Kieve. Ziara ya viongozi hao inafanyika wakati Ukraine ikizidi kuyashinikiza mataifa ya Magharibi kwa ujumla wake yairuhusu kutumia makombora ya masafa marefu dhidi ya Urusi.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW