Serikali ya mpito ya Haiti yasema imeiomba Marekani kupeleka wanajeshi wake nchini humo kulinda miundo mbinu muhimu, Polisi nchini Bangladesh yawakamata watu wanane kwa mashtaka ya mauaji yanayohusiana na moto uliozuka katika kiwanda kimoja na kuwauwa kiasi cha watu 52 na bomu lililotegwa ndani ya gari lawauwa watu wanane mjini Mogadishu nchini Somalia