1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Mashambulizi ya wanamgambo yawaua watu 33 Pakistan

26 Agosti 2024

Watu 33 wameuawa katika msururu wa mashambulizi yanayowalenga maafisa wa polisi kusini magharibi mwa Pakistan, raia na wasafiri.

https://p.dw.com/p/4jvDm
Pakistan Balochistan | Uharibifu uliofanywa na watu wenye silaha nchini Pakistan
Uharibifu uliofanywa na watu wenye silaha nchini Pakistan.Picha: STR/AFP/Getty Images

Kulingana na msemaji wa eneo hilo Shahid Rind mapema leo, magaidi walianzisha mashambulizi katika maeneo matatu tofauti yaliyolenga reli, bomba la gesi na vituo vya polisi.

Karibu watu 23 waliuawa alfajiri ya leo baada ya watu waliokuwa na silaha kuwalazimisha abiria kushuka kwenye treni na mabasi, kukagua utambulisho wao na kuwaua wote waliotokea jimbo la Punjab.

Abiria waliouliwa katika wilaya ya Musakhail, ambako washambuliaji waliweka vizuizi kwenye barabara kubwa inayokutanisha majimbo na kuchoma magari.

Watu wengine 10, polisi watano na raia watanowaliuliwa kwenye wilaya ya Kalat, amesema Ihsanullah Khan, wa jeshi la polisi la eneo hilo.