1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya mabomu Uganda yaibua wasiwasi

Lubega26 Oktoba 2021

Kisa kingine cha mripuko wa bomu kimezidisha hofu na wasiwasi nchini Uganda licha ya serikali kuendelea kutoa hakikisho kuwa watakabiliana na vitisho hivyo vinavyotajwa kuwa vya kigaidi.

https://p.dw.com/p/42BiF

Vifo vya abiria wawili jana wakati bomu liliporipuka kwenye basi vinaleta mashaka ya usalama kama anavyoripoti mwandishi wetu Lubega Emmanuel kutoka Kampala.

Kulingana na taarifa za polisi, bomu hilo liliripuka mwendo wa saa kumi jioni kwenye basi lililokuwa likielekea kusini magharibi mwa nchi.

Abiria wawili walifariki papo hapo huku 37 wakinusurika kifo kwa kupata majeraha. Hali hii imeibua wasiwasi miongoni mwa watu waliopanga kwenda safari:

Huku polisi ikiahidi kuchunguza madai ya kundi la kigaidi la ISIS kufanya mashambulizi haya Uganda idadi ya waliopoteza maisha yao katika muda wa siku mbili wamefikia wanne sasa.

Sasa raia wenyewe wanachukua tahadhari ya kuhakikisha kwamba wanaepuka na meaneo yenye misongamano ya watu.

Je, mashambulizi ya mabomu Uganda yachochewa na nini?

Kwa upande wake, serikali imepanga kutoa taarifa zaidi kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa kuepusha mashambulizi hayo ya mabomu inayodai ni vitendo vya makundi yaliyo na mafungamano na waasi wa ADF ambao wanaendesha mashambulizi dhidi ya raia nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hadi wakati wa kuandaa ripoti hii, serikali ilikuwa imeahidi kutoa taarifa rasmi kuhusu shambulio hilo la pili. Shambulio la kwanza lilitokea siku ya Jumamosi.