1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel ndani ya Syria yawaua watu 5

9 Septemba 2024

Mashambulizi ya anga ya Israel yaliyoyalenga maeneo matano ndani ya Syria yamesababisha vifo vya watu wasiopungua watano.

https://p.dw.com/p/4kPhR
Ndege ya jeshi la Israel| Syria
Ndege ya jeshi la Israel.Picha: IMAGO/ZUMA Press Wire

Hayo yametangazwa na vyombo vya habari vya Syria pamoja na shirika linalofuatia Haki za Binadamu nchini humo.

Taarifa zinasema ndege za kivita za Israel ziliyalenga maeneo ya kijeshi kwenye jimbo la Hama lililopo magharibi mwa Syria. Mkurugenzi wa hospitali ya serikali kwenye eneo hilo amesema mbali ya watu watano waliouawa, wengine 19 wamejeruhiwa na baadhi yao wako kwenye hali mahututi.

Israel imekuwa ikifanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Syria kwa kile inachosema ni kuzuia kutanuka kwa ushawishi wa kijeshi kutoka Iran na makundi ya watu wenye silaha inayoyafadhili.