1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Libya yaelekeza mashambulizi miji ya magharibi

3 Juni 2023

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya (GNU) jana Ijumaa imeripotiwa kuongeza mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya kile ilichosema kukabiliana na magenge ya magendo katika mikoa ya magharibi

https://p.dw.com/p/4S9JK
Libyen | Interims-Premierminister Abdelhamid Dbeibah
Picha: Mahmud Turkia/AFP

Hata hivyo, mashambulizi hayo yaliyoanza wiki moja iliyopita yamepiga kiwanda kinacho husishwa na mpinzani maarufu wa Waziri Mkuu  Abdelhamid al-Dbeibah, hatua ambayo imesababisha chuki kwa wanaoikosoa serikali na kuzusha hofu ya vurugu kuongezeka zaidi.

Marekani na nchi nyingine za Magharibi zimepaza sauti ya hofu kutokana na matumizi ya silaha katika maeneo ya raia wa Zawia na kuwataka viongozi kutuliza hali hiyo.