1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yawawekea vikwazo "waliochangia" mapigano Kongo

25 Agosti 2023

Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo watu sita inaosema walichangia kuchochea mapigano ya hivi karibuni katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4VZbs
DR Kongo Soldaten
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya fedha ya Marekani, waliowekewa vikwazo ni raia wa Rwanda na Kongo kutoka makundi ya wanamgambo au jeshi wanaoatjwa kuhusika na mapigano na "ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu."

Miongoni mwa hao raia wa Rwanda ni Apollinare Hakizimana na Sebastian Uwibambazi wote wakiwa ni viongozi wa kundi la FDLR la Rwanda.

Soma zaidi:Marais wa jumuiya ya SADC waidhinisha kupelekwa jeshi Kongo
Marekani yazitaka Rwanda, Kongo kuutuliza mvutano

Raia wa Kongo waliowekewa vikwazo ni Bernard Byamungu, ambaye ni kiongozi katika kundi la waasi la M23, na Salomon Tokolonga kutoka kwenye jeshi la Kongo.

Vikwazo hivyo vimepelekea mali zao zilizoko Marekani kufungiwa na ni sharti ziripotiwe.