1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatangaza msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine

Josephat Charo
30 Julai 2024

Marekani imetangaza msaada mpya wa kijeshi wa thamani takriban dola bilioni 1.7 kwa ajili ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4itnu
Ukraine | Uwasilishaji wa vifaa vya kijeshi
Wafanyakazi wakipakua shehena ya misaada ya kijeshi iliyotolewa kama sehemu ya usaidizi wa usalama wa Marekani kwa Ukraine, katika uwanja wa ndege wa Boryspil, nje ya Kyiv, Januari 25, 2022.Picha: Efrem Lukatsky/AP/picture alliance

Msaada huo unajumuisha silaha na risasi ambazo vikosi vya Ukraine vinasema vinazihitaji sana kwa dharura. Wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, imesema katika taarifa kuwa msaada huo unajumuisha vifaa vya thamani ya dola milioni 200 vitakavyotolewa kutoka kwa shehena za sasa za kijeshi za Marekani na vitafika uwanja wa vita haraka, pamoja na vifaa vingine vipya vilivyoagizwa ambavyo vitachukua muda mrefu zaidi kuwasili. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyamesema katika taarifa aliyoituma kwenye mtandao wa kijamii kwamba anamshukuru rais wa Marekani Joe Biden, bunge la Marekani na watu wa Marekani kwa msaada huo.