Marekani yashinikiza kuondolewa kwa ripoti kuhusu njaa Gaza
27 Desemba 2024Shirika linalofuatilia mizozo ya chakula duniani, FEWS NET, linalofadhiliwa na Marekani, limeondoa ripoti yake iliyotahadharisha kuhusu baa la njaa linalokaribia kaskazini mwa Gaza kutokana na mzingiro wa Israel, baada ya Marekani kuomba iondolewe, kufuatia ukosoaji kutoka kwa Balozi wa Marekani nchini Israel, Jacob Lew.
Hatua ya serikali ya Biden kupinga ripoti hiyo, ambayo inapaswa kutoa tathmini isiyoegemea upande wowote kuhusu mizozo ya chakula, imeibua wasiwasi miongoni mwa mashirika ya misaada na haki za binadamu kuhusu kuingiliwa kisiasa.
Soma pia: Mashirika ya kimataifa yaonya juu ya kitisho cha njaa zaidi
Ripoti hiyo ilikadiria vifo vya njaa kaskazini mwa Gaza kufikia watu 2-15 kwa siku ifikapo Machi iwapo sera hazitabadilika. Marekani ilikosoa matokeo hayo kama yasiyo sahihi, ikitaja hali inayobadilika Gaza, huku maafisa wa misaada wakisisitiza uzito wa hali hiyo kutokana na uchache wa misaada inayowafikia waathirika na vita vinavyoendelea.