1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaonya Urusi kuwa makini katika urushaji ndege zake

15 Machi 2023

Maafisa wa Marekani wamemuambia balozi wa Urusi nchini Marekani kuwa Moscow inapaswa kuwa makini wakati inarusha ndege zake katika anga ya kimataifa. Msemaji wa Ikulu ya Marekani John Kirby amesema hayo leo.

https://p.dw.com/p/4Oiff
USA Kommunikationsdirektor Nationaler Sicherheitsrat John Kirby
Picha: ANDREW CABALLERO-REYNOLDS/AFP

Marekani imeweka wazi hayo kufuatia kuangushwa kwa droni ya kijeshi ya Marekani katika Bahari Nyeusi baada ya kukatizwa na ndege za kivita za Urusi.

Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani ilimuita balozi wa Urusi mjini Washington, Anatoly Antanov, kuelezea wasiwasi wa Marekanikuhusu tukio hilo, ambalo ni la kwanza tangu vita vya nchini Ukraine kuanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Soma pia:Droni ya Marekani yaanguka baharini, Urusi yaombwa maelezo

Urusi imeonya dhidi ya kile ilichokiita uhasama wa ndege za Marekani huku balozi Antonov akisema wanatumai Marekani itajizuia kutoa uvumi zaidi katika vyombo vya habari na kukoma kurusha ndege karibu na mipaka ya Urusi.