1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yakamilisha ujenzi wa bandari ya muda Gaza

16 Mei 2024

Wanajeshi wa Marekani wamekamilisha bandari ya muda katika pwani ya Gaza , iliyokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu, ili kuongeza kasi ya kufikisha misaada katika ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4futx
Zypern Larnaca |  Nahrungsmittelhilfe der US-amerikanischen Hilfsorganisation World Central Kitchen
Picha: Getty Images/AFP/Hasan Mroue

Wanajeshi wa Marekani wamekamilisha bandari ya muda katika pwani ya Gaza , iliyokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu, ili kuongeza kasi ya kufikisha  misaada katika ukanda wa Gaza.

Soma: Vita vya Gaza: Blinken akutana na Netanyahu

Katika mtandao wa kijamii wa X, Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani inayounga mkono operesheni ya kupeleka msaada wa ziada wa kibinadamu kwa raia wa Palestina wanaohitaji, imesema malori ya kupeleka msaada yataanza kusonga mbele kwenye pwani hiyo leo.

Ujenzi wa bandari hiyo ya muda ulitangazwa  mwezi Machi na Rais Joe Biden na kujengwa kwa gharama ya takriban dola milioni 320, ni sehemu ya juhudi za kimataifa za kukwepa vizuizi vya ardhini kuingia katika Ukanda wa Gaza vilivyowekwa na Israel, mshirika wa karibu wa Washington.Wakaazi wa Rafah wako hatarini kushambuliwa na Israel

Haya yanajiri huku Israel ikidai kuwa wanajeshi wake watano wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa ufyatulianaji risasi katika vita vya Gaza.

Kwa mujibu wa jeshi watano hao waliuawa wakati vifaru viwili vya Israel vilirusha makombora kwa makosa katika jengo walimokuwa wakati wa mapigano katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa nchi hiyo siku ya Jumatano.