1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yahimiza haki za wafanyakazi wa bandarini

Josephat Charo
2 Oktoba 2024

Ikulu ya Marekani imesema wakati umewadia kwa muungano wa vyama vya waajiri wa wafanyakazi wa bandarini, United States Maritime Alliance (USMX) kufanya mazungumzo ya kuandaa mikataba ya haki kwa wafanyakazi wao.

https://p.dw.com/p/4lKEW
Marekani | bandarini
Wafanyakazi wa bandarini wa Marekani wakiandamana kudai haki zao.Picha: Spencer Platt/Getty Images

Wito huo umetolewa wakati wafanyakazi wa bandarini katika pwani ya mashariki na pwani ya ghuba ya Marekani wakianza mgomo wao wa kwanza mkubwa kabisa katika kipindi cha miaka 50.

Msemaji wa ikulu ya Marekani, Karine Jean-Pierre, amesema kampuni za meli zimefanikiwa kuweka rekodi kwa kupata faida tangu janga la korona na baadhi zimeshuhudia faida zao zikikua kupita kiwango cha asilimia 800 ikilinganishwa na faida zao kabla janga hilo.

Soma zaidi: Watu 600 hawajulikani walipo North Carolina

Malipo ya marupurupu kwa wakuu wa makampuni hayo imeongezekana kutokana na faida hizo na wamiliki wa hisa nao pia wamenufaika sana.

Jean-Pierre amesema ni haki kwa wafanyakazi wanaohatarisha maisha yao kuhakikisha bandari zinaendelea kufanya kazi wapate nyongeza ya maana katika mishahara yao.