1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yabaini uhalifu wa kivita katika vita vya Sudan

7 Desemba 2023

Marekani imesema jana kwamba vikosi pinzani nchini Sudan kwa pamoja vimefanya uhalifuwa kivita katika mzozo baina yao.

https://p.dw.com/p/4ZrkQ
Tschad | Menschen auf der Flucht vor der Gewalt in West Darfur überqueren die Grenze
Picha: Zohra Bensemra/REUTERS

Washington aidha imedai kuwepo kwa kampeni ya safishasafisha ya kikabila katika jimbo la Darfur,Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasilisha ripoti hiyo iliyotokana na uchunguzi uliofanywa na wizara yake, baada ya miezi kadhaa ya kuongezeka wasiwasi na mazungumzo kushindwa kutoa suluhu.Blinken amesema majeshi yote mawili ya Sudan na wanamgambo wa RSF, yamefanya uhalifu wa kivita, na kuongeza kuwa RSF pia wamefanya safishasafisa ya kikabila na uhalifu dhidi ya ubinaadamu akiangazia mauaji ya watu wengi dhidi ya jamii ya Masalit, huko Darfur.Blinken ameyataka majeshi hayo kumaliza mzozo sasa na kuzingatia wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu, na kuwawajibisha wale wanaohusika na ukatili.