1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani, Uingereza na Australia kutengeza kombora la kisasa

6 Aprili 2022

Uingereza, Australia na Marekani zimekubaliana kushirikiana kutengeza makombora ya kisasa. Ikulu ya White House, imesema wanataka kuharakisha utengenezaji huo na kufanyia kazi ulinzi dhidi ya silaha za kisasa.

https://p.dw.com/p/49We8
Israel I  Israeli Arrow 3 Rakete
Picha: Israeli Defence Ministry/AFP

Makombora hayo hufikia zaidi ya mara tano ya kasi ya sauti na bado yanaweza kubadilika wakati wa kuruka. Makombora ya aina hii ni vigumu kuyazuwia. Na kama ilivyo kwa makombora ya masafa marefu, makombora haya ya kasi kubwa zaidi yanaweza pia kuwekewa vichwa vya nyuklia. China imeripotiwa kulifanyia majaribio kombora la aina hii kwa ufanisi mwaka jana, na Urusi imefahamisha kwamba imetumia kombora kama hilo katika vita vyake dhidi ya Ukraine.