1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Ripoti za mauaji Mali zinasikitisha 

4 Aprili 2022

Marekani imesema inafuatilia taarifa za kutatanisha kuhusu idadi ya watu wengi waliouawa nchini Mali.

https://p.dw.com/p/49QDu
USA Ukraine-Russland-Konflikt | Pressesprecher Ned Price
Picha: Tom Brenner/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Ned Price amesema jana kuwa kuna taarifa za kutatanisha kuhusu waliohusika na mauaji hayo yaliyotokea mwishoni mwa mwezi Machi katika kijiji cha Moura, umbali wa kilomita 400 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Mali, Bamako.

Price amesema wana wasiwasi kwamba ripoti nyingi zinaonesha wahalifu walikuwa wapiganaji wa kampuni binafsi ya kijeshi ya Urusi ya Wagner Group.

Amesema taarifa nyingine zinadai kuwa Jeshi la Mali, FAMa, limewalenga wahusika wa makundi yenye itikadi kali ambayo yanajulikana. Siku ya Jumamosi, jeshi la Mali lilisema kwamba limewaua zaidi ya wapiganaji 200 wenye itikadi kali za Kiislamu.

Maafisa katika ubalozi wa Urusi nchini Marekani wamekataa kuzungumzia taarifa za kuhusika kwa Wagner Group katika mauaji hayo.