1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Marekani na Urusi zatoa mwito wa utulivu Nagorno Karabakh

20 Septemba 2023

Urusi na Marekani, zimetoa rai ya kupunguzwa mvutano kwenye mzozo kati ya Azerbaijan na Armenia, siku moja baada ya Azerbaijan kuanzisha operesheni ya kijeshi kwenye jimbo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh.

https://p.dw.com/p/4WZxF
Athari za vita vya Nagorno-Karabakh
Azerbaijan na Armenia zimeshapigana vita mbili kuwania udhibiti wa Nagorno-KarabakhPicha: Oldhike/TASS/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Antony Blinken amesema amezungumza na marais wa nchi hizo mbili na kumrai rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan kusitisha mara moja hatua zote za kijeshi kwenye jimbo hilo lenye mzozo.

Kwa upande wake Urusi, ambayo mpatanishi wa jadi wa mzozo huo wa miongo kadhaa, imezihimiza pande zote mbili kusitisha mapigano na kumaliza uhasama.

Baada ya miezi kadhaa ya mivutano kwenye eneo la Nagorno-Karabakh linalodhitiwa na Waarmenia, Azerbaijan ilituma vikosi vyake jana kwa dhamira ya kulirejesha jimbo hilo chini ya udhibiti wake.

Mzozo kuhusu jimbo hilo unapindukia miaka 30 na nchi hizo mbili jirani zimeshapigana vita mbili kuwania udhibiti wake ikiwemo ya mnamo mwaka 2020.