1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Uingereza zaipa Ukraine msaada wa $ bil. 1.5

Angela Mdungu
12 Septemba 2024

Uingereza na Marekani zimeahidi kuipa Ukraine nyongeza ya msaada wa karibu dola bilioni 1.5 za Kimarekani. Ahadi hiyo imetolewa wakati wa ziara ya Mawaziri wa masuala ya kigeni wa nchi hizo mbili nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4kXdt
Wanadiplomasia wa ngazi za juu wa Ukraine, Marekani na Uingereza.
Wanadiplomasia wa ngazi za juu wa Ukraine, Marekani na Uingereza.Picha: Mark Schiefelbein Pool via REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema nchi yake itatoa zaidi ya dola 700 kwa ajili ya msaada wa kiutu wakati mwenzake wa Uingereza akisema David Lammy akithibitisha msaada wa zaidi ya dola milioni 600 kwa Ukraine.

"Msaada huo ni pamoja na dola milioni 242 kwa mwaka huu ukiwa ni msaada wa haraka wa kushughulikia maswala ya kibinadamu, mahitaji ya umeme, pamoja na kusaidia hatua za mageuzi, kujikwamua na ujenzi mpya."

Soma pia:US, UK kutafakari ombi la Kyiv kulegeza vikwazo vya kutumia silaha zao ndani ya Urusi

Ziara hiyo ya Kidiplomasia inafanyika wakati jeshi la Urusi likiendelea kufanya mashambulizi katika miji mingi ya Ukraine kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani hali ambayo imeshasababisha vifo vya raia wengi.